Waziri Balozi Kombo atembelea Maonesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar (ZITF) 2026

ZANZIBAR-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb) ametembelea Maonesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar (ZITF) 2026 yanayoendelea katika Kituo cha Maonesho cha Zanzibar, Dimani.
Maonesho hayo yalianza Disemba 29, 2025 yatamalizika Januari 16, 2026 ni maalum kwa ajili ya maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Alipofika katika viwanja vya maonesho hayo, Mhe. Waziri Kombo alitembelea pia Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kupokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar pamoja na wafanyakazi wa Wizara walioko katika ofisi hiyo

Maonesho hayo yanalenga kuangazia fursa za biashara na uwekezaji ndani na nje ya nchi.
Taasisi mbalimbali za serikali kutoka Zanzibar na Tanzania Bara zinashiriki katika maonesho hayo na kutoa fursa ya kuelimisha umma juu ya huduma na bidhaa mbalimbali ambazo zinatolewa na kuzalishwa na taasisi hizo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here