Wizara ya Madini,taasisi wajadili utekelezaji wa ahadi zake bungeni mwaka 2025/26

DODOMA-Katibu Mkuu Wizara ya Madini,Eng. Yahya Samamba ameongoza kikao cha Menejimenti ya Wizara na Taasisi zake kupitia na kujadili hatua za utekelezaji wa Ahadi zilizotolewa Bungeni na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde wakati akiwasilisha Hotuba yake kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.
Katika Mwaka wa Fedha 2025/26, Wizara ya Madini pamoja na kuweka mikakati ya kutekelezwa, ilipanga kutekeleza vipaumbele mbalimbali ikiwemo kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali; kuongeza mchango wa Sekta kwenye Pato la Taifa; kuhamasisha uwekezaji na uongezaji thamani madini; kuimarisha uendelezaji minada na maonesho ya madini ya vito, kuongeza uwekezaji kwenye tafiti zake za kina; kuwarasimisha wachimbaji wadogo na kuzijengea uwezo taasisi zake.

Akizungumza katika kikao hicho, Eng. Samamba amesisitiza kutekelezwa kikamilifu kwa ahadi zilizotolewa na Wizara ili kuendelea kuongeza tija kwa taifa kupitia rasilimali madini.
Naye, Katibu Mtendaji Tume ya Madini Eng. Ramadhan Lwamo amesema tayari mzabuni atakayesimamia minada ya kimataifa ya Madini ya vito amekwishapatikana.

Kufanyika kwa minada ya kimataifa ya Madini ya vito pamoja na mambo mengine kutaongeza mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa kupitia fedha za kigeni, kuitangaza Tanzania na madini yake yanayopatikana nchini, kuvutia uwekezaji zaidi, kuimarisha hadhi ya Tanzania kimataifa kupitia minada hiyo ya madini ya vito, kuwepo kwa bei halisi ya soko, uwazi na kuongeza washiriki wa ndani na kimataifa.
Manufaa mengine ni pamoja na kukuza wachimbaji wa ndani, masoko ya uhakika ya madini ya vito na bei za uhakika.

Pamoja na masuala mbalimbali yaliyojadiliwa, taarifa ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) imeeleza kuhusu hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa kiwanda cha kusafisha chumvi katika Mkoa wa Lindi ambapo imeeleza kwamba matarajio ni kuwa ifikapo mwezi Februari, 2026 kiwanda hicho kitaanza kazi na hivyo kuondoa changamoto ya soko kwa wazalishaji wa chumvi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here