Balozi Mwamweta na Mheshimiwa Mtaka wasaka soko la parachichi Ujerumani

BERLIN-Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Hassani Iddi Mwamweta anaongoza ujumbe wa wakulima na wafanyabiashara kutoka Tanzania unaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Matunda na Mbogamboga ya Fruit Logistica 2026 yanayofanyika Berlin kuanzia Februari 03 hadi 06, 2026.
Ujumbe huo unajumuisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Bw. Saleh Saad Mohamed unatumia maenesho hayo kupata fursa ya kutanua masoko kwa kuongeza masoko mapya, kuongeza mtandao wa wafanyabiashara na kujifunza maarifa mapya kuhusu kilimo-biashara.
Kampuni zaidi ya 40 kutoka Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi za TAHA, Mamlaka ya Udhibiti Nafaka na Mazao Mchanganyika (COPRA) na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wameshiriki Maonesho hayo ambayo yamehudhuriwa na kampuni zaidi ya 2600 kutoka nchi 151 duniani.
Fruits Logistica ni Maonesho ya Kimataifa ya Matunda na Mbogamboga ambayo huwaleta pamoja wakulima, wasambazaji, wanunuzi, wasafirishaji na wadau mbalimbali katika mnyororo wa usambazaji wa matunda na mbogamboga kutoka duniani kote.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here