Magazeti leo Februari 13,2026

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limekifunga kiwanda cha kutengeneza zege cha JUYE Concrete Company Ltd kilichopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam, kufuatia tuhuma za uchafuzi wa mazingira unaowaathiri wakazi wa maeneo jirani.
Zuio hilo limetolewa Februari 12, 2026, na Meneja wa Uzingatiaji wa Sheria wa NEMC, Hamadi Taimuru, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kiwandani hapo kukagua utekelezaji wa maagizo yaliyokuwa yametolewa awali.

Kwa mujibu wa Taimuru, kiwanda hicho kilianza kukaguliwa tangu mwaka jana na kimepewa maelekezo mara nne ili kurekebisha kasoro zilizobainika. Hata hivyo, malalamiko kutoka kwa wakazi wa karibu kuhusu vumbi na maji taka yameendelea kuripotiwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here