Watumishi sita wa Idara ya Afya katika Halmashauri ya Wilaya Kigoma mkoani Kigoma wamefariki baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kutoka Kigoma Mjini kuelekea Kijiji cha Kagunga, Halmashauri ya Wilaya Kigoma kwa shughuli ya kutoa chanjo kukumbwa na dhoruba Ziwa Tanganyika na kupinduka.




Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa Kigoma, Michael Maganga alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili asubuhi Machi 13, 2026 Kijiji cha Kalalangabo Manispaa ya Kigoma Ujiji na kwamba miili hiyo sita imepatikana.


Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo










