Ushirikiano wa Tanzania na Japan waongeza nguvu Sekta ya Zimamoto

TOKYO-Machi 17,2026, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Japan, Mheshimiwa Anderson Mutatembwa alipokea kwa niaba ya Serikali msaada wa magari matatu ya zimamoto na uokoaji yaliyotolewa na Taasisi ya Zimamoto ya Japan (Japan Firefighters Association).
Magari hayo ni sehemu ya magari Matano ambayo Taasisi hiyo imepanga kuipatia Tanzania mwaka 2026 na yanatarajiwa kuwasili nchini mwezi Mei 2026.
Msaada huo ni sehemu ya mpango wa taasisi hiyo wa kutoa magari 30 ndani ya kipindi cha miaka mitano hadi mwaka 2028 ukilenga kuimarisha huduma za zimamoto na uokoaji nchini na kuongeza uwezo wa nchi kukabiliana na majanga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here