DAR-Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 29 inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake Alhamisi ya Aprili 23,2026 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Othman Chande, wakati akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam.
Tume hiyo imesema, ripoti hiyo itakuwa msingi muhimu wa kutoa mwelekeo kuhusu matukio hayo.
