Waziri Kombo akutana na Balozi wa Denmark,waazimia kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia

DAR-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amefanya mazungumzo na Balozi wa Denmark nchini, Mhe. Jesper Kammersgaard, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Denmark.
Mazungumzo hayo yamefanyika Aprili 27, 2026, katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi hao wamekubaliana kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa pande mbili katika sekta mbalimbali za maendeleo, zikiwemo uwekezaji, afya na kilimo.
Aidha, wamesisitiza umuhimu wa kuendeleza mahusiano ya kidiplomasia na kupanua wigo wa ushirikiano katika sekta za kimkakati kwa manufaa ya mataifa yote mawili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here