Magazeti leo Mei 12,2026

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekutana na wadau kutoka sekta mbalimbali kwa lengo la kujadili namna ya kuboresha ukusanyaji wa mapato pamoja na kuimarisha utendaji kazi wa mamlaka hiyo.
Mkutano huo umefanyika Mei 11, 2026 jijini Dar es Salaam ukilenga kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili wadau katika utekelezaji wa majukumu yao ya kikodi, sambamba na kutafuta suluhisho la changamoto hizo kwa pamoja.

Aidha, TRA imeeleza kuwa vikao vya aina hiyo vitaendelea kufanyika kila baada ya miezi mitatu ili kutoa nafasi kwa wadau kuwasilisha maoni yao na kujadili maboresho mbalimbali yanayohusu huduma za kodi nchini.

Akizungumza katika mkutano huo, Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda amesema mamlaka hiyo itaendelea kutoa elimu kwa walipakodi, kuboresha mifumo ya utoaji huduma pamoja na kuhakikisha utekelezaji wa maazimio yaliyojadiliwa unaanza mara moja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here