Magazeti leo Mei 13,2026

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha bajeti ya Wizara ya Afya ya Shilingi trilioni 1.8 kwa mwaka wa fedha 2026/27, ikiwa ni hatua muhimu katika kuendelea kuimarisha huduma za afya nchini.
Bajeti hiyo iliyowasilishwa na Waziri wa Afya, Mh. Mohammed Mchengerwa inalenga kuongeza ubora wa huduma za afya, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, kuendeleza miundombinu ya hospitali pamoja na kusogeza huduma bora kwa wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.

Kati ya fedha zilizopitishwa, Shilingi trilioni 1.148 sawa na asilimia 64 zitaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo huku Shilingi bilioni 652.236 zikitumika kwa matumizi ya kawaida ya wizara hiyo.

Aidha, kupitia bajeti hiyo serikali itaendelea kusimamia maboresho makubwa katika sekta ya afya ikiwemo ujenzi wa hospitali, vituo vya afya, upatikanaji wa wataalamu pamoja na kuimarisha huduma za kibingwa na ubingwa bobezi nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here