Manchester United yamtangaza Michael Carrick kuwa Kocha Mkuu wa kudumu

NA DIRAMAKINI

KLABU ya Manchester United imemtangaza rasmi Michael Carrick kuwa kocha mkuu wa kudumu wa timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili utakaomuweka katika dimba la Old Trafford hadi mwaka 2028.
Uamuzi huo umefikiwa na uongozi wa United baada ya kuridhishwa na kiwango cha mafanikio alichokionesha Carrick tangu alipokabidhiwa jukumu la kuinoa timu hiyo kwa muda.

Katika kipindi chake cha uongozi wa muda, Carrick ameiongoza Manchester United kurejea katika ushindani wa UEFA Champions League baada ya timu hiyo kumaliza msimu katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.

Mbali na hilo, kocha huyo ameonesha uwezo mkubwa wa kiufundi kwa kupata matokeo chanya dhidi ya baadhi ya vigogo wa Premier League, jambo lililoongeza imani kwa mabosi wa klabu hiyo.

Uongozi wa Manchester United unaamini Carrick ana uwezo wa kuirejesha klabu hiyo katika ubora wake wa zamani na kuwania tena mataji makubwa ndani na nje ya England.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here