Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete aongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Bajeti ya EAC

ARUSHA-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete tarehe 22 Mei, 2026 jijini Arusha ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Mawaziri kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkutano huo ni hatua muhimu ya maandalizi ya Bajeti ya Jumuiya hiyo kabla ya kuwasilishwa katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kwa ajili ya kujadiliwa na kuidhinishwa kabla ya Juni 30,2026.
Katika mkutano huo, Mhe. Ridhiwani Kikwete aliambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki, Cde. James Millya; Naibu Waziri wa Fedha Cde. Mshamu Ali Munde; Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Kaimu Katibu Mkuu anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa; pamoja na maafisa wengine waandamizi wa Serikali.

Aidha, katika Mkutano huo wamejadili mipango ya kibajeti ya Taasisi mbalimbali ikiwemo Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki, Bunge la Afrika Mashariki, Taasisi ya Bonde la Ziwa Victoria na nyinginezo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here