Serikali yateua viongozi wa Kamati za Usalama Barabarani mikoa yote 31

DAR-Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud amefanya uteuzi wa Wenyeviti, Wajumbe na Makatibu wa Kamati za Usalama Barabarani katika mikoa yote 31 ya Kipolisi nchini.
Uteuzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam ukiwa na lengo la kuimarisha mfumo wa usimamizi wa usalama barabarani na kuhakikisha kuwa mikakati ya kuzuia ajali inatekelezwa kwa ufanisi

​Akizungumza mara baada ya kutia saini orodha ya Viongozi wa Kamati hizo katika kikao kazi na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza, SACP William Mkonda amesema hatua hiyo ni sehemu ya dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhakikisha usalama wa watumiaji wa barabara unaimarika na kupunguza ajali zinazoweza kuepukika.

Uteuzi huu umezingatia kikamilifu Sheria ya Usalama Barabarani, Sura ya 168 (R.E 2023), Sehemu ya VII, kuanzia kifungu cha 110 hadi 113, ambavyo ndivyo vinavyotoa mamlaka ya kuundwa kwa Baraza la hilo. 

Aidha, Mhe. Ayoub ametumia mamlaka aliyopewa chini ya Kanuni ya 15 ya Kanuni za Baraza (TS Namba 392/1986), inayompa Mwenyekiti uwezo wa kutoa maelekezo ya utekelezaji wa majukumu ya Baraza hilo kisheria.

Kadhalika kikao hicho kilikuwa ni sehemu ya Maandalizi ya kikao kijacho cha Baraza la Taifa la Usalama barabarani. 

Uteuzi huu wa viongozi wa mikoa unakuja kufuatia hatua ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Patrobas Katambi, kumteua Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here