MSD yaibuka kinara katika matumizi ya Mfumo wa NeST

ARUSHA-Bohari ya Dawa (MSD) imeendelea kuthibitisha ubora wake katika usimamizi wa ununuzi wa umma baada ya kutunukiwa Tuzo ya Utendaji Bora katika Ununuzi wa Umma na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).
MSD imetambuliwa kama Taasisi Bora kwa Ujumla katika Matumizi ya Mfumo wa Kitaifa wa Ununuzi wa Umma kwa Njia ya Kielektroniki (NeST) kwa mwaka wa fedha 2025/2026, ikiwa ni uthibitisho wa uwazi, ufanisi na matumizi sahihi ya teknolojia katika utekelezaji wa shughuli za ununuzi wa umma.

Tuzo hiyo ilikabidhiwa hapo jana tarehe *29 Julai 2026, wakati wa Kongamano la 10 la Kitaifa la Ununuzi wa Umma, linaloendelea katika Ukumbi wa AICC mkoani Arusha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here