PPAA yawaita wadau ununuzi wa umma katika Maonesho ya Sabasaba kupata elimu

DAR-Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imewasihi wadau wa ununuzi wa umma na wananchi kwa ujumla kutembelea banda la Mamlaka ya Rufani kupata uelewa juu ya majukumu na huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo hususan matumizi ya Moduli ya kupokea na kushughulikia malalamiko na rufaa katika mfumo wa NeST.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Sehemu ya Huduma za Sheria PPAA, Bi. Agnes Sayi kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando. Bi Sayi alitoa wito huo leo tarehe 01 Julai, 2026 katika Banda la Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba).
Pamoja na mambo mengine, PPAA katika maonesho hayo inatoa elimu kuhusu uamuzi juu ya rufaa zinazotokana na mchakato wa ununuzi wa umma, uamuzi juu ya rufaa zinazotokana na kufungiwa kushiriki katika michakato ya ununuzi wa umma pamoja na uamuzi juu ya malalamiko yanayotokana na kushindwa kwa Afisa Masuuli kutoa uamuzi ndani ya muda uliowekwa.

“Maeneo mengine yanayotolewa elimu ni uamuzi juu ya malalamiko baada ya mkataba wa ununuzi kuanza kutekelezwa, uamuzi juu ya maombi ya kuongezewa muda wa kuwasilisha rufaa nje ya muda uliowekwa, uamuzi juu ya maombi ya utekelezaji wa amri ya Mamlaka ya Rufani, uamuzi juu ya maombi ya kufuta uamuzi uliotolewa bila kusikiliza upande mwingine (Ex Parte decision) na uamuzi juu ya maombi ya kurejesha rufaa,” amesema Bi. Sayi.
Maonesho hayo yameanza tarehe 28 Juni yataendelea hadi 13 Julai 2026 katika Viwanja vya Mwl. Nyerere Jijini Dar es Salaam. Aidha, Taasisi mbalimbali za Umma zimeshiriki maonesho hayo kwa lengo la kuonesha huduma wanazotoa kwa wananchi kwa kaulimbiu: Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba, Fahari ya Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here