Waziri Mkuu akagua maandalizi ya Siku ya Mashujaa

DODOMA-Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, Julai 17, 2026 amekagua na kupokea taarifa ya maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yanayotarajiwa kufanyika Julai 25, 2026 katika Viwanja vya Mashujaa, Mtumba, jijini Dodoma.
Katika ukaguzi huo, Waziri Mkuu ameridhishwa na hatua zilizofikiwa na kuwataka wote wanaohusika kuendelea kukamilisha maandalizi yaliyobaki kwa wakati ili maadhimisho hayo yafanyike kwa utaratibu na hadhi inayostahili.
Maadhimisho hayo yataongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here