Balozi Yakubu asisitiza umuhimu wa Olduvai na Ngorongoro-Lengai katika urithi wa utalii Tanzania

ARUSHA-Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania UNESCO, Mhe. Saidi Yakubu, amesema Ngorongoro–Lengai UNESCO Global Geopark na Olduvai Gorge ni miongoni mwa hazina za kipekee zinazoipa Tanzania nafasi muhimu duniani katika historia ya mwanadamu, sayansi ya jiolojia, uhifadhi na utalii wa urithi.
Katika ziara hiyo, Balozi Yakubu aliambatana na Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO Tanzania, Dkt. Khamis Khalid Said, pamoja na maafisa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Akiwa Ngorongoro, Balozi Yakubu alikutana na Mhifadhi Mkuu wa Ngorongoro, Kamishna Abdulrazak Badru, Naibu Mhifadhi Joan Makwati, Mkuu wa Makumbusho ya Geopark Dkt. Agness Gidna, pamoja na Mkuu wa Kituo cha Olduvai Gorge, Ikayo Sambeta.

Aliwapongeza viongozi na wataalamu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) kwa weledi, maarifa na juhudi zao katika kuhifadhi, kutafiti na kuutangaza urithi huu muhimu kwa Tanzania na dunia.
Balozi Yakubu amesisitiza kuwa hadhi ya UNESCO inapaswa kuendelea kuwa kichocheo cha ushirikiano wa kimataifa katika uhifadhi, utafiti wa kisayansi, mafunzo, teknolojia na kubadilishana maarifa, huku wataalamu wa Kitanzania wakiendelea kuwa kiini cha juhudi hizo.

Amesema Olduvai Gorge na Ngorongoro–Lengai zinapaswa kuendelea kuwa kinara cha utalii na urithi wa Tanzania duniani, zikivutia wageni si kwa mandhari na wanyamapori pekee, bali pia kwa historia ya mwanadamu, sayansi, utamaduni na urithi wa kipekee unaopatikana katika ardhi ya Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here