BoT yanzindua rasmi kielelezo cha faida rejea ya Dhamana za Serikali

NA DIRAMAKINI

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),Bw. Emmanuel Tutuba amezindua rasmi kielelezo cha faida rejea ya dhamana za serikali lengo likiwa ni kuleta uwazi katika soko la ndani la dhamana za serikali na kuboresha upatikanaji wa bei halisi za soko, huku akisema kwamba dhamana zisizoifa zimeongezeka kutoka shilingi bilioni 499 hadi kufikia trilioni 32.291 kwa mwaka 2026.
Amesema,hatua hiyo itaboresha mfumo mzima wa uwekezaji na kwenda sambamba na upanuzi wa wigo kwa wawekezaji wa nje na ndani katika sekta ya fedha.

Akizindua kielelezo hicho leo Agosti 7,2026 jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Gavana Tutuba amesema wawekezaji katika masoko ya kifedha wameongezeka kutoka wawekezaji 897 hadi kufikia wawekezaji 32,631 hivi sasa.

Amesema kuwa,idadi hiyo ya wawekezaji bado ni ndogo sana ikilinganishwa na idadi ya watanzania lzaidi ya milioni 61 tuliopo.
Aidha,amewataka wadau wa kifedha waungane ili waweze kuangalia fursa ambazo hazijafikiwa ili wawekezaji waweze kuwekeza huko

"Fursa zipo nyingi sana na hazijafikiwa,hivyo ni vizuri wadau wote wa sekta ya fedha kuungana ili zile fursa ambazo hazijafikiwa zifikiwe," amesema Tutuba.

Amesema kuwa, katika kipindi cha miaka miwili wameongeza ukwasi wa takribani shilingi trilion 10 kwenye mzunguko.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA),CPA. Nicodemus Mkama amesema,uzinduzi wa kielelezo hicho ni hatua za kimkakati cha kuchochea ukuaji wa dhamana za serikali na kuchuja miamala isiyo ya kawaida.

Amesema kuwa, soko liko salama na linaendelea kukua na kwamba uwekezaji umekuwa kwa asilimia 45 na kwa upande wa soko la hisa uwekezaji umefikia asilimia 79 na kwa hati fungani ni asilimia 48.

Naye, Mkurugenzi wa Madalali wa Fedha, Godfrey Malauli amesema,bado kuna kazi ya kujenga uelewa kwa wawekezaji kuhusiana na masuala mbalimbali ya uwekezaji kwenye sekta hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here