Magazeti leo Agosti 25,2026

Serikali imekutana na wamiliki wa Viwanda vya kuzalisha pombe kali nchini ikiwa ni hatua ya kuendelea kupambana na bidhaa bandia na duni.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb) kukutana na kufanya mazungumzo na wamiliki wa Viwanda vya pombe kali Agosti 24, 2026 jijini Dar es Salaam, katika kikao kilicholenga kutafuta suluhu ya changamoto hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Kapinga amesisitiza umuhimu wa mzalishaji wa pombe kali kuendelea kuzingatia Sheria, taratibu na kanununi za uanzishwaji wa Viwanda hivyo, kwa kuzingatia ubora, usafi na afya ya mtumiaji.















Hatua hiyo inatajwa kuwa sehemu ya jitihada za Serikali za kuhakikisha mazingira ya biashara yanakuwa rafiki huku wananchi wakipata bidhaa muhimu na halali kwa bei inayokubalika.

Kikao hicho pia kimeweka mkakati wa pamoja wa kila mzalishaji wa pombe kali kuendelea kutoa Elimu kwa wadau na Wananchi ili kutofautisha bidhaa bandia na halali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here