MOROGORO-Kuelekea Tamasha la Nne la Kitaifa la Utamaduni mkoani Morogoro kwa mwaka 2026, mkoa huo umeanza shamrashamra kwa matukio ya kukaribisha na kuhamasisha wananchi kushiriki tamasha hilo linaloanza Agosti 25 hadi 29,2026 katika Uwanja wa Jamhuri.
Ambapo Agosti 24, 20226 limefanyika bonanza la michezo likiwa na jina la Utamaduni Jogging likijumuisha mbio fupi pamoja michezo mbalimbali ikiwemo riadha, kuvuta kamba, kutembea na mayai kwenye kijiko pamoja na kutembea kwa magunia.Mgeni rasmi katika tukio hilo akiwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Mhe. Khalid Matengo ameongoza bonanza hilo ambalo pia limehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Methusela Ntonda.
Pamoja na washindi wa Bonanza hilo kupewa medali, pia wamehamasishwa kuendelea kushiriki michezo mara kwa mara ili kuimarisha afya zao.
Tags
Bonanza la Michezo
Habari
Michezo
Morogoro Region
Sanaa na Utamaduni
Tamasha la Utamaduni Kitaifa
















