Watumishi wa Wizara ya Fedha wapewa elimu ya kinga na utambuzi wa saratani

NA JORDAN MBWAMBO

WIZARA ya Fedha kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani Ocean Road imeanza kutekeleza zoezi la utoaji wa elimu kuhusu saratani pamoja na vipimo vya uchunguzi wa awali wa saratani kwa watumishi wa Wizara hiyo ili kuongeza uelewa wa namna ya kujikinga, kutambua dalili za awali na kuchukua hatua stahiki kukabiliana na ugonjwa huo.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha wakifuatilia elimu iliyokuwa inatolewa na wataalamu kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, kuhusu namna ya kujikinga, kutambua dalili za awali na kuchukua hatua stahiki katika kukabiliana na ugonjwa wa saratani, katika zoezi linalofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Mtumba, jijini Dodoma, kuanzia tarehe 10 hadi 14 Agosti 2026.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma).

Zoezi hilo litakalohusisha utoaji wa elimu kuhusu saratani mbalimbali, ikiwemo saratani ya matiti, tezi dume na shingo ya kizazi, pamoja na vipimo vya awali linatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 10 hadi 14 Agosti 2026, katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Mtumba, jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Chotto Sendo, akizungumza katika zoezi la utoaji wa elimu kuhusu saratani pamoja na vipimo vya uchunguzi wa awali wa saratani kwa watumishi wa wizara hiyo, linalofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Mtumba, jijini Dodoma, kuanzia tarehe 10 hadi 14 Agosti 2026.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mali za Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Chotto Sendo, alisema ni muhimu kwa watumishi kufuatilia elimu ya afya ya saratani ili kuwa na uelewa wa kutosha kukabiliana na ugonjwa huo.

‘‘Ni muhimu kuwa na uelewa sahihi kuhusu saratani, hususan kwa kuzingatia kwamba utambuzi wa ugonjwa huo katika hatua za awali una nafasi kubwa katika matibabu na kuokoa maisha,"alisema Bw. Sendo.
Afisa Utumishi Mwandamizi, Wizara ya Fedha, Bw. Salum Said, akifafanua jambo katika zoezi la utoaji wa elimu kuhusu saratani pamoja na vipimo vya uchunguzi wa awali wa saratani kwa watumishi wa Wizara hiyo, linalofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Mtumba, jijini Dodoma, kuanzia tarehe 10 hadi 14 Agosti 2026.
Daktari Bingwa wa Saratani kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dkt. Frank Ruta, akitoa elimu kuhusu kinga, utambuzi na matibabu ya saratani kwa watumishi wa Wizara ya Fedha, katika zoezi linalofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Mtumba, jijini Dodoma, kuanzia tarehe 10 hadi 14 Agosti 2026.

Aliwasisitiza watumishi wa Wizara hiyo kutumia fursa hiyo kupata elimu pamoja na kufanya vipimo vya awali vinavyotolewa ili kufahamu hali zao za afya.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Saratani, Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dkt. Frank Ruta, aliwahimiza watumishi hao kutopuuza mabadiliko au dalili zisizo za kawaida katika miili yao na kufika katika vituo vya afya kwa ajili ya uchunguzi na ushauri wa kitaalamu.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha wakifuatilia elimu iliyokuwa inatolewa na wataalamu kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, kuhusu namna ya kujikinga, kutambua dalili za awali na kuchukua hatua stahiki katika kukabiliana na ugonjwa wa saratani, katika zoezi linalofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Mtumba, jijini Dodoma, kuanzia tarehe 10 hadi 14 Agosti 2026.

Alisema,utambuzi wa saratani katika hatua za awali unaongeza nafasi ya mafanikio ya matibabu, hivyo jamii inapaswa kujenga utamaduni wa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara na kuchukua hatua za mapema katika kuzuia na kukabiliana na saratani.

Dkt.Ruta alisemna elimu hiyo ni sehemu ya jitihada za kuimarisha uelewa wa watumishi na jamii kwa ujumla kuhusu afya na kuwahamasisha kuchukua hatua za mapema katika kuzuia na kukabiliana na saratani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here