ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Benki ya Dunia katika kuimarisha sekta za elimu, afya, nishati na miundombinu, huku akisisitiza kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili wananchi wanufaike kwa wakati.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Agosti 19,2026 alipokutana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Afrika Mashariki na Kusini, Dkt. Ndiamé Diop aliyeambatana na Mkurugenzi wa Divisheni ya Benki hiyo anayesimamia Malawi,Tanzania, Zambia na Zimbabwe, Bw. Firas Raad katika mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Zanzibar.Miongoni mwa waliohudhuria mazungumzo hayo ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ndg. Khamis Abdulla Said, pamoja na viongozi na watendaji wengine wa Serikali na Benki ya Dunia.
Amesema,Serikali itaendelea kuimarisha uwekezaji katika sekta za kipaumbele, kutoa fursa kwa Sekta Binafsi na kuimarisha mafunzo ya amali ili vijana wapate ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira.
Tags
Benki ya Dunia (WB)
Benki ya Dunia Tanzania
Dkt.Hussein Ali Mwinyi
Habari
Kimataifa
Zanzibar News

