Nina imani na uwezo wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amempongeza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,Abdi Mahmoud Abdi kwa uteuzi wake na kumtaka kutekeleza majukumu yake kwa bidii huku akiahidi kumpatia ushirikiano zaidi.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Agosti 19,2026 alipokutana na Bw.Abdi Mahmoud Abdi aliyefika Ikulu Zanzibar kujitambulisha rasmi kufuatia uteuzi wake kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, pamoja na kupokea maelekezo kuhusu utekelezaji wa majukumu yake mapya.
Amesema,ana imani na uwezo wake kutokana na uzoefu na utendaji aliouonesha alipokuwa Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, huku akisisitiza umuhimu wa kushirikiana na viongozi na watendaji wa Chama katika kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar, Bw. Abdi Mahmoud Abdi amemshukuru Rais Dkt. Mwinyi kwa ushauri na maelekezo aliyompatia, na kuahidi kufanya kazi kwa bidii na kushirikiana na viongozi na watendaji wenzake katika kutekeleza majukumu ya Chama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here