Aliyekuwa Afisa wa Polisi Mrakibu wa Polisi (SP) Frank Mwasampili azikwa jijini Mbeya

MBEYA-Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga ameshiriki katika maziko ya aliyekuwa Afisa wa Polisi Mrakibu wa Polisi (SP) Frank Mwasampili aliyefariki dunia Septemba 21, 2026 katika ajali iliyotokea mkoani Singida.
Marehemu SP Frank Mwasampili alikuwa akifanyia kazi Mkoa wa Singida na amezikwa Septemba 23, 2026 nyumbani kwao Kijiji cha Imezu kilichopo Mkoa wa Mbeya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ametoa pole kwa familia kwa msiba mzito wa kuondokewa na mpendwa wao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here