Chemba wasalimisha silaha haramu kwa hiari

DODOMA-Wananchi wilayani Chemba Mkoa wa Dodoma wamejitokeza kwa hiari kusalimisha silaha haramu ambazo walikuwa wanazimiliki kinyume cha sheria katika vituo mbalimbali vya Polisi na ofisi za serikari za mitaa ambapo hakuna hatua zozote za kisheria zitakazochukuliwa dhidi yao.
Mara baada ya kupokea silaha hizo Septemba 11, 2026, Mkuu wa Kituo cha Polisi Chemba Mrakibu wa Polisi,SP Robert Mwakikunga, amesema,kitendo hicho kimeonesha uzalendo wa kweli katika kutii sheria na kanuni za nchi.

SP Mwakikunga amewataka wananchi hao kuwa mabalozi wazuri kwa wengine katika kuhamasisha wanachi wengine ambao wamekuwa wakimiliki silha kinyume cha Sheria waweze kuzisalimisha silaha hizo kwa hiari yao wenyewe.
Aidha, wananchi hao wameishukuru Serikali pamoja na Jeshi la Polisi kwa kutoa msamaha huo,kwani umewapa nafasi ya kusalimisha silaha bila kuchukuliwa hatua yoyote ya kisheria huku wakiahidi kuendelea kutoa ushirikano wa kufichua uhalifu na wahalifu katika Jamii

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here