Mafunzo ya Makanda Wakufunzi ni muhimu kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi (CCM)- Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, mafunzo ya makada wakufunzi ni muhimu katika kuimarisha chama kuanzia ngazi za chini, kwa kuhakikisha misingi, itikadi, historia na maadili ya CCM vinaeleweka na kufikishwa kwa wanachama kwa usahihi.
Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo Septemba 30, 2026 wakati akifunga Mafunzo ya Wakufunzi wa Makada wa CCM Awamu ya Pili yaliyofanyika Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema, jumla ya makada 840 wamepatiwa mafunzo kupitia programu hiyo, huku akiwataka wakufunzi hao kuimarisha elimu ya Chama, matumizi ya teknolojia ya kidijitali, pamoja na kuimarisha mashina na matawi katika kusikiliza na kushughulikia kero za wanachama na wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here