Waziri Mkuu akutana na viongozi wa madereva, mgomo wasitishwa

DAR-Waziri Mkuu, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba leo Septemba 30,2026 amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa madereva wa mabasi na malori nchini, katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamekubali kusitisha mgomo wa madereva uliodumu kwa siku mbili, hatua inayowezesha huduma za usafiri kuendelea kama kawaida.
Aidha, Serikali imeeleza utayari wake wa kusikiliza na kufanyia kazi changamoto zinazowakabili madereva, kwa lengo la kupata suluhisho la masuala yaliyosababisha mgomo huo.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha huduma za usafiri zinaendelea kutolewa huku majadiliano kuhusu changamoto za madereva yakiendelea kati ya Serikali na wadau husika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here