Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (MB), amezitaka taasisi za elimu ya juu nchini kuimarisha tafiti, ubunifu na matumizi ya sayansi na teknolojia ili kutoa suluhisho la changamoto zinazoikabili jamii na kuchangia maendeleo ya endelevu.
Masauni ametoa rai hiyo Septemba 24, 2026, wakati akifunga rasmi Mkutano wa Tatu wa Muungano wa Vyuo Vikuu Vitano (Five Universities Consortium), uliofanyika katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela ya Afrika (NM-AIST), Arusha.
Amesema vyuo vikuu havipaswi kubaki kuwa vituo vya kuzalisha maarifa pekee, bali vinapaswa kuwa vitovu madhubuti vya utatuzi wa changamoto, kwa kuunganisha utafiti, sayansi, teknolojia, sera, sekta binafsi na mahitaji ya jamii.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo

















