Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Pili wa Doha (DOHA DIALOGUE) kuhusu uhamaji wa nguvu kazi na ajira, unaotarajiwa kufanyika Oktoba 5 na 6, 2026, jijini Dar es Salaam, ukiwa na lengo la kukuza fursa za ajira kwa Watanzania nje ya nchi.
Mkutano huo utafanyika katika hotel ya Hyatt Regency na kuwakutanisha zaidi ya nchi 33 kutoka Afrika, nchi za Ghuba, Jordan na Lebanon kujadili namna ya kuimarisha uhamaji wa nguvu kazi na ajira zenye staha.Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu–Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amesema Tanzania ni nchi ya pili kuwa mwenyeji wa Doha Dialogue na ya kwanza barani Afrika.
Amesema mkutano huo utajadili mikataba ya ajira baina ya nchi, uanishaji wa ujuzi na mahitaji ya soko la ajira, pamoja na maandalizi ya wafanyakazi kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo




















