BRELA yatoa notisi ya mwisho ya nia ya kufuta kampuni 5,277 katika Daftari la Msajili

NA DIRAMAKINI

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umeutaarifu umma kuwa, Msajili wa Kampuni ametoa Notisi ya Mwisho ya Nia ya Kufuta Kampuni katika Daftari la Msajili, kwa mujibu wa kifungu cha 403(3) cha Sheria ya Kampuni, Sura ya 212.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Septemba 28,2026 na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano na Umma.

"Hatua hii imekuja baada ya Msajili kutoa Notisi mbili za awali kwa kampuni husika, ambapo Notisi ya kwanza ilitolewa tarehe 2 Juni 2022 na Notisi ya pili tarehe 13 Julai 2022. Kupitia Notisi hizo, kampuni zilizoorodheshwa zilitakiwa kuthibitisha iwapo zinaendelea kufanya biashara."

Kwa mujibu wa Notisi ya Mwisho iliyotolewa kwenye Gazeti la Serikali Toleo Na 38 la tarehe 18 Septemba, 2026, kampuni zote zilizoorodheshwa kwenye gazeti hilo zimepewa muda wa siku tisini (90) kuanzia tarehe ya tangazo hilo kuwasilisha pingamizi kwa Msajili wa Kampuni dhidi ya nia ya kufutwa kwake.

"BRELA inawataka Wakurugenzi, Wanahisa na Makatibu wa kampuni zilizoorodheshwa kuchukua hatua stahiki ndani ya muda uliotolewa, kwa kuwa endapo hakutatokea pingamizi lolote baada ya muda wa siku tisini (90) kumalizika, Msajili ataendelea na hatua za kuzifuta kampuni hizo kutoka katika Daftari la Msajili."

Orodha ya kampuni zinazokusudiwa kufutwa Soma kwa kina hapa

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here