Mtendaji wa Kijiji cha Igombavanu ahukumiwa kwa kuiba fedha za kijiji

MUFINDI-Aliyekuwa Afisa Mtendaji wa Kijiji (VEO) cha Igombavanu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa,Deus Mathias Mbilinyi amehukumiwa kifungo cha nje cha miezi sita pamoja na kulipa fidia kwa Serikali kiasi cha shilingi 500,000.
Kesi hiyo ya Jinai Namba 14272/2026 kati ya JAMHURI dhidi ya Deus Mathias Mbilinyi imeamriwa leo Septemba 16,2026 katika Mahakama ya Wilaya ya Mufindi mbele ya Mheshimiwa Bennedict Nkomola, Hakimu Mkazi Mfawidhi.

Mshtakiwa ametiwa hatiani baada ya kukiri kosa la wizi akiwa mtumishi wa umma kinyume na kifungu cha 258(1),(2) (a) na 270 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16, marejeo ya mwaka 2023 na kuhukumiwa kifungo cha nje pamoja na kuilipa Serikali fidia.

Ilibainika kuwa,kati ya Juni Mosi,2021 na Juni 6,2021 mshtakiwa aliiba jumla ya Shilingi 840,000 ikiwa ni asilimia 10 ya fedha ya mapato ya kijiji katika mauziano ya shamba ekari 24 alilouziwa, Bi.Magret Jacob Mkusa katika Kijiji cha Igombavanu na muuzaji Mario Gabriel Mkalimoto iliyopaswa kuwekwa kwenye Akaunti ya Benki ya Kijiji cha Igombavanu.

Aidha,mshtakiwa amerejesha kiasi chote cha fedha Shilingi 840,000 kwenye Akaunti ya kijiji hicho ikiwa ni asilimia 10 ya bei ya mauziano ya shamba hilo Shilingi 8,400,000.

Kesi hiyo imeendeshwa na Mawakili wa Serikali, Kassim Mussa, Lissa Kasongwa na Salum Bhoki kutoka Ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) Mkoa wa Iringa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here