NECTA yatangaza ratiba ya upimaji wa darasa la nne Oktoba,2026

NA DIRAMAKINI

BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza ratiba ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne kwa mwaka 2026, huku wanafunzi wakitarajiwa kufanya upimaji huo katika masomo mbalimbali kuanzia Oktoba 5 hadi 6, 2026.
Ratiba hiyo imetolewa na baraza hilo leo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia huku ikiainisha muda wa kufanya upimaji, namba za mificho pamoja na masomo yatakayofanyiwa upimaji katika siku hizo mbili.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, upimaji utaanza Jumatatu, Oktoba 5, 2026, kwa wanafunzi kufanya masomo kadhaa katika vipindi tofauti.

Saa 2:00 hadi 3:30, wanafunzi watafanya upimaji wa Jiografia na Mazingira: Sanaa na Michezo, wenye namba ya mficho A06, huku somo la Geography and Environment: Arts and Sports likiwa na namba A06E.

Baada ya hapo, kuanzia saa 3:30 hadi 4:30, kutakuwa na kipindi cha mapumziko.

Kuanzia saa 4:30 hadi 6:00, wanafunzi watafanya Hisabati, yenye namba ya mficho M08, pamoja na Mathematics yenye namba M08E.

Kipindi kingine cha mapumziko kimepangwa kuanzia saa 6:00 hadi 8:00, kabla ya wanafunzi kufanya Sayansi kuanzia saa 8:00 hadi 9:30. Somo hilo lina namba za mificho S09 na S09E.

UPIMAJI WA JUMANNE

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, siku ya pili ya upimaji itakuwa Jumanne, Oktoba 6, 2026.

Siku hiyo, wanafunzi wataanza na Kiswahili kuanzia saa 2:00 hadi 3:00, kikiwa na namba ya mficho L01.

Kipindi cha mapumziko kitafuata kuanzia saa 3:00 hadi 4:00, kabla ya wanafunzi kufanya English Language kuanzia saa 4:00 hadi 5:00, ikiwa na namba ya mficho L02.

Baada ya hapo, kutakuwa na mapumziko ya dakika 30, kuanzia saa 5:00 hadi 5:30.

Kuanzia saa 5:00 hadi 5:30, ratiba imeainisha kipindi cha mapumziko, huku kuanzia saa 5:30 hadi 6:30 wanafunzi wakifanya masomo ya lugha, ambayo ni French Language, Lugha ya Kiarabu na Lugha ya Kichina, yenye namba za mificho L03, L04 na L05, mtawalia.

Baada ya masomo hayo, wanafunzi watakuwa na mapumziko kuanzia saa 6:30 hadi 8:00.

Upimaji wa mwisho kwa siku hiyo utafanyika kuanzia saa 8:00 hadi 9:30, ambapo wanafunzi watafanya Historia ya Tanzania na Maadili, yenye namba ya mficho A07.

WADAU WATAKIWA KUZINGATIA RATIBA

Ratiba hiyo rasmi imeainisha kwa utaratibu muda wa kuanza na kumalizika kwa kila somo, pamoja na vipindi vya mapumziko, hivyo shule, walimu, wanafunzi na wazazi wanapaswa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Baraza la Mitihani.

Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne ni miongoni mwa hatua zinazotumika katika kutathmini maendeleo ya wanafunzi katika ujifunzaji na kutoa taarifa muhimu kuhusu kiwango cha uelewa wa masomo wanayofundishwa.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, masomo yaliyopangwa kufanyiwa upimaji ni Jiografia na Mazingira: Sanaa na Michezo, Hisabati, Sayansi, Kiswahili, English Language, French Language, Lugha ya Kiarabu, Lugha ya Kichina pamoja na Historia ya Tanzania na Maadili.

Baraza la Mitihani la Tanzania limeweka ratiba hiyo ikiwa na marejeo SFNA 2026, huku upimaji ukifanyika katika kipindi cha siku mbili, Oktoba 5 na 6, 2026.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here