Uhamiaji Simiyu washiriki zoezi la usafi mwisho wa mwezi

SIMIYU-Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Simiyu imeendelea kushiriki zoezi la usafi wa mazingira mwishoni mwa mwezi, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa kushirikiana na Serikali pamoja na wananchi katika kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama.
Zoezi hilo limeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga ambaye amekuwa akisisitiza umuhimu wa usafi wa mazingira na kutajwa kama kinara wa usafi katika Wilaya ya Bariadi.
Zoezi hilo limefanyika katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Bariadi, ambapo watumishi wa Idara ya Uhamiaji walishiriki kikamilifu katika usafi wa mazingira, hatua inayolenga kuimarisha usafi na kujiandaa kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Maafisa na Askari wa Idara ya Uhamiaji waliongozwa na Afisa Uhamiaji Wilaya ya Bariadi, Mrakibu Mwandamizi Vera Paul Mwasha, ambaye alishiriki pamoja na watumishi wengine katika zoezi hilo.
Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Simiyu itaendelea kushirikiana na Serikali za Mitaa na wananchi katika shughuli mbalimbali zenye lengo la kulinda mazingira, afya na ustawi wa jamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here