ROMA-Waziri Mkuu,Dkt. Mwigulu Nchemba amewasili jijini Roma nchini Italia leo Septemba 20, 2026 kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Kimataifa wa Afya Moja na Mifumo ya Chakula na Kilimo (One Health), utakaofanyika Septemba 21–23, 2026 katika Makao Makuu ya FAO.
Akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Leonardo da Vinci (Fiumicino), Waziri Mkuu amepokelewa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ngwaru Maghembe; na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk.
Tags
Afya Moja
Dr Mwigulu Lameck Nchemba
FAO
Habari
Mifumo ya Chakula na Kilimo
Picha
Picha Chaguo la Mhariri






