DAR ES SALAAM- Makumbusho ya Taifa la Tanzania jijini Dar es Salaam imeendelea kutekeleza jukumu lake la mashirikiano ya kidiplomasia, kuhifadhi na kuendeleza kumbukumbu za kihistoria kwa kupokea ziara ya Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mheshimiwa William Trachman.
Balozi huyo ametembelea mnara wa kumbukumbu wa “Matumaini baada ya Huzuni” na kuweka shada la maua kwa heshima ya waathirika wa mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea Agosti 7, 1998 katika balozi za Marekani nchini Tanzania.
Ziara ya Balozi Trachman imekuja siku chache baada ya kupokelewa kwa Hati zake za Utambulisho na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 15 Oktoba 2026.
Hatua hiyo inaashiria mwendelezo wa mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Marekani, ambayo pia yanajengwa katika misingi ya ushirikiano wa kulinda amani na kupinga vitendo vya ugaidi.
Makumbusho ya Taifa la Tanzania ina jukumu muhimu la kukusanya, kuhifadhi, kutafiti, kutoa elimu na kutangaza urithi wa taifa, ikiwemo kumbukumbu za matukio yanayogusa historia ya nchi na mahusiano yake na mataifa mengine.
Tags
Balozi William Trachman
Dar es Salaam
Habari
Kimataifa
Kumbukumbu ya Ugaidi 1998
Makumbusho ya Taifa la Tanzania
Uhusiano wa Tanzania na Marekani
Ushirikiano wa Kidiplomasia




