Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 20, 2026

Soma habari zote muhimu leo Oktoba 20, 2026 kutoka katika magazeti makubwa ya Tanzania kama Mwananchi, HabariLeo, Majira, Nipashe, Zanzibar Leo, Raia Mwema, Mwanahalisi, Uhuru, Pambazuko, Jamhuri na mengineyo kila siku bila malipo.
Gazeti la MWANANCHI leo Jumanne Oktoba 20, 2026 habari kuu ni siku mbili za vilio, simanzi: Jinamizi la Mauaji: Askari 13 mbaroni mauaji ya watu wanne Kagera. Mtoto amuua baba, naye auawa: Ndejembi atoa mwelekeo kuziinua kampuni changa. Mahakama yaipiga stop kamati ya mawakili sakata la Mwabukusi.
Gazeti la HABARI LEO leo Jumanne Oktoba 20, 2026 habari kuu ni Neema yaja wenye kampuni changa, Ndejembi atoa miezi sita sera: Tril 3.9 zatengwa elimu. HABARI LEO michezo habari kuu ni Ndejembi kulea mpira wa kikapu: Watanzenia wang'ara marathoni Nagai: Mashabiki kuishuhudia Simba Mwembeyanga kesho.
Gazeti la JAMHURI leo Jumanne Oktoba 20, 2026 habari kuu ni kuhusu Jeuri ya pesa, Hifadhi ya Barabara Morogoro yajengwa vituo vya mafuta: Bima yakua kwa asilimia 68. JAMHURI michezo habari kuu ni Drogba: Fursa isipotee bure, Morogoro yajipanga kwa SHIMMUTA: Yanga ilishinda 4-0.
Gazeti la Majira leo Jumanne, Oktoba 20, 2026 habari kuu ni Tanzania, IFC kushirikiana katika mageuzi ya kiuchumi. Makamu wa Rais aipa miezi sita Wizara ya Viwanda na Rais Hichilema azifunda nchi Ukanda wa Maziwa Makuu. Majira, upande wa michezo ni Makamu wa Rais ashuhudia fainali mpira wa kikapu. Dar City yatwaa ubingwa kwa kuichapa Stein Warriors 66-50, na mashabiki kuitazama Simba, 15de Agosto kwenye kioo.
Gazeti la Nipashe leo Jumanne Oktoba 20, 2026 habari kuu ni Chakula chaua. Watoto 41 waliokula baada ya utamaduni, mmoja afariki. Saa 17 kuzima moto ghala la dawa, vifaa tiba vya binadamu. Nipashe Michezo, habari kuu ni Simba kwa mara ya nne kukosa mashabiki. Manqoba: Yanga SC imepata suluhisho. Tanzania yabeba medali nne za dhahabu.
Gazeti la UHURU leo Jumanne Oktoba 20, 2026 habari kuu ni Ujumbe wa Rais Samia mtihani kidato cha nne. Ndejembi atoa siku 180 sera maalumu. Askari mbaroni tuhuma mauaji. UHURU Michezo habari kuu ni Ndejembi mlezi mpira wa kikapu. Dar City washinda vikapu 66-50. Simba yajipanga ndani, nje ya uwanja CAFCC.
Zanzibar Leo, leo Jumanne Oktoba 20, 2026 habari kuu ni Othman: Wapeni elimu waumini kuhusu hijja. Serikali itaendelea kushirikiana na wakulima wa karafuu. Mitihani ya kidato cha nne yaanza kwa utulivu.
Tanzania Leo, leo Jumanne Oktoba 20, 2026: Watanzania waamka Samia akiwapigania. Askari 13 mbaroni tuhuma vifo Kagera. Ndejembi atoa miezi 6 sera vijana. Tanzania Leo Spoti, Jumanne Oktoba 20, 2026: Ndejembi aziota Simba, Yanga. TFF kuvuna Sh 2.4 Bil kutoka Caf. Drogba ajionea maandalizi ya Afcon Mkapa.
Gazeti la Daima Tanzania leo Jumanne, Oktoba 20, 2026 habari kuu ni Benki ya Dunia yaelezea imani yake kwa uchumi wa Tanzania, IFC yaahidi kuendelea kusaidia. Waziri Mkuu awasili Marekani kumwakilisha Rais Samia, na Diwani wa Msigani aipongeza Shule ya St Anne Marie Academy, ni kwa kuwa shule pekee nchini kusomesha bure wanaofiwa na wazazi.
Gazeti la Raia Mzalendo leo Jumanne Oktoba 20, 2026 habari kuu ni Biashara ya Kaboni yaanza kuingiza mamilioni. Wilaya ya Tanganyika yavuna zaidi ya shilingi milioni 700, kujenga Kituo cha Afya cha Katuma: Dk Mwigulu awasili Marekani kumwakilisha Rais Samia, Serikali yaweka mipango kuwainua boda boda kiuchumi, IFC yaahidi kuisaidia Tanzania.
Gazeti la Biashara Leo, leo Jumanne Oktoba 20, 2026 habari kuu ni Washirika wa maendeleo wazidi kuiamini Tanzania. IFC laahidi kuipiga jeki Dira 2050 na kuchangia mpango wa Central Corridor: Waziri Masauni asema Wilaya ya Tanganyika ni mfano wa kuigwa biashara ya Kaboni, imeshavuna milioni 700 kujenga kituo cha afya.
Gazeti la Mwananchi Huru leo Jumanne Oktoba 20, 2026 habari kuu ni Wananchi Katavi wamshukuru Rais Samia kwa mradi wa kaboni. Wasema umeimarisha uhifadhi wa mazingira na kuwanufaisha: Tanzania na IFC kushirikiana katika mageuzi ya kiuchumi. Waziri Omar azungumza na Makamu wa Rais wa shirika hilo, Bangkok.
Gazeti la WAMACHINGA leo Jumanne Oktoba 20, 2026 habari kuu ni Askari 13 washikiliwa tuhuma za mauaji Kagera. Waziri wa Afya apiga marufuku dawa zisizosajiliwa kulipwa bima. WAMACHINGA katika ukurasa wa michezo habari kuu ni Makamu wa Rais sasa mlezi mpira wa kikapu. Simba, De Agosto sasa jino kwa jino. Himid Mao azivutia timu Ligi Kuu.
Gazeti la MwanaHabari leo Jumanne Oktoba 20, 2026 habari kuu ni Serikali yaanza kusukuma sera maalum ya startups, Makamu wa Rais azungumzia umuhimu wa sera hiyo: MAMCU yauza korosho tani 30,000. MwanaHabari katika ukurasa wa michezo habari kuu ni Ndejembi akubali kuwa mlezi mpira wa kikapu: Simba tutajaza uwanja mechi ya marudiano na Yanga yaita mashabiki Chamazi.
Taifa Tanzania leo Jumanne Oktoba 20, 2026: Ndejembi ataka sera ya biashara bunifu. Tanzania na IFC kushirikiana mageuzi kiuchumi. Polisi washikilia askari 13 tuhuma mauaji. Taifa Tanzania Michezo, Jumanne Oktoba 20, 2026: Makamu wa Rais: Serikali itaendelea kuwekeza kwenye michezo. Simba SC yaweka wazi mchezo dhidi ya FC 15 de Agosto bila mashabiki.
MWANA SPOTI leo Jumanne Oktoba 20, 2026: Kibano cha madawa Ligi Kuu, Rais TFF atangaza mkakati mpya. Ndejembi anogeshea fainali ya kikapu Dar. Manqoba ajifungia na kiungo Yanga SC. Mo atoa maagizo Simba. UEFA leo tena, Bayern vs Arsenal kesho saa 4:00 usiku.
SAUTI YETU leo Jumanne Oktoba 20, 2026: Tanzania, IFC kushirikiana mageuzi ya Kiuchumi, ukuaji Sekta Binafsi. Balozi Omar: Sekta Binafsi tegemeo Dira 2050. Ndejembi atoa miezi sita Wizara ya Viwanda kuandaa sera bunifu, lengo kufungua fursa za kiuchumi kwa vijana. Shilingi Bilioni 98 MAMCU LTD ikiuza korosho tani 30,000.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here