CAP yaitaka Korea Kusini kulinda haki za Kiongozi wa Shincheonji, Lee Man-hee

GENEVA-Shirika la CAP Liberté de Conscience limelitaka Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuishinikiza Serikali ya Korea Kusini kuhakikisha haki za Mwenyekiti wa Kanisa la Shincheonji la Yesu, Lee Man-hee (95) anayeshikiliwa akisubiri kesi zinalindwa.
Mwenyekiti wa Kanisa la Shincheonji la Yesu, Lee Man-hee (95) anayeshikiliwa kizuizini.

Katika taarifa iliyotolewa Septemba 18, 2026, mjini Geneva, Uswisi, shirika hilo lilieleza wasiwasi kuhusu mazingira ya kizuizini ya Lee, likidai kuwa alihifadhiwa katika sero zisizo na kiyoyozi wakati wa joto kali.

CAP pia imedai kuwa, uchunguzi dhidi ya kiongozi huyo unaonekana kuwa na msukumo wa kisiasa na kulenga kundi la kidini la wachache.

Limeitaka Serikali ya Korea Kusini kuzingatia haki za binadamu, kuruhusu tathmini huru ya kitabibu na kuhakikisha kesi yake inaendeshwa kwa haki na bila upendeleo.
CAP Liberté de Conscience ni shirika lisilo la kiserikali linalotetea uhuru wa dini na imani na kupinga ubaguzi unaotokana na dini au imani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here