Dabi: Serikali yaruhusu Uwanja wa Uhuru, mazoezi marufuku

NA DIRAMAKINI

WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetangaza kuwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam upo tayari kwa mchezo wa Dabi ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga utakaopigwa Oktoba 10, 2026.
Hata hivyo, Wizara imesisitiza kuwa uwanja huo hautatumika kwa mazoezi ya timu zozote mbili kuelekea mchezo huo.

Kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa Oktoba 7, 2026 jijini Dodoma na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Bi. Zaituni Mkwama, Wizara imeeleza kuwa, hatua hiyo ni kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa na Bodi ya Ligi kuhusu matumizi ya viwanja vya mashindano.

"Ifahamike kua kuelekea mchezo huo Uwanja wa Uhuru hautatumika kwa mazoezi na timu yoyote kati ya hizo mbili, kwa kuzingatia matakwa ya kifungu husika cha kanuni za mashindano ya ligi," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Wizara imewataka wadau wote wa soka, mashabiki wa Simba na Yanga na umma kwa ujumla kuzingatia utulivu, amani na taratibu zilizowekwa wakati wakisubiri mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na Watanzania wote.

Mchezo wa Dabi ya Kariakoo unatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam baada ya uwanja huo kufanyiwa ukarabati na kutangazwa kuwa tayari kwa matumizi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here