Kapinga akabidhi mbegu za kahawa kilo 1,000 kwa AMCOS 20 Mbinga

RUVUMA-Mbunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini ambaye ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Judith Kapinga amekabidhi kilo 1,000 za mbegu za kahawa kwa AMCOS 20 na kikundi kimoja ili kuzalisha vitalu vya miche ya kahawa ili kuzalisha miche milioni 3.5 na kuendeleza jitihada za kuzalisha kahawa wilayani humo.
Amekabidhi mbegu hizo leo Oktoba 07, 2026 wakati wa ziara yake alipotembelea Halmashauri ya Mbinga iliyopo katika jimbo hilo.

Mheshimiwa Kapinga amesema, uchumi wa halmashauri hiyo ni kilimo cha kahawa, kwani msimu uliopita halmashauri hiyo imezalisha tani 18,000 na kwa msimu huu imepanga kuzalisha tani 19,000 ambapo mpaka sasa imevuka malengo hayo kabla ya msimu kuisha.
Waziri Kapinga ameongeza kuwa, utoaji wa mbegu hizo ni kuchagiza uzalishaji wa kahawa kwa wingi ili kuchochea uchumi kwa wananchi wa Mbinga pamoja na upatikanaji wa mapato kwa halmashauri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here