Rais Dkt. Mwinyi: SMZ kufadhili wanafunzi 143 wa Kidato cha Sita

ZANZIBAR- Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itafadhili masomo ya shahada ya kwanza kwa wanafunzi 143 waliofanya vizuri katika Mitihani ya Taifa ya Kidato cha Sita mwaka 2026, kupitia Mpango wa Ufadhili wa Masomo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ Scholarship).
Aidha, amesema Serikali imeongeza bajeti ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kutoka shilingi bilioni 35 mwaka wa fedha 2025/2026 hadi shilingi bilioni 45 mwaka wa fedha 2026/2027, sawa na ongezeko la takriban asilimia 29.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 21 Oktoba 2026, katika hafla ya kuwapongeza wanafunzi waliofanya vizuri katika Mitihani ya Taifa ya Kidato cha Nne na Sita kwa miaka ya 2024, 2025 na 2026, iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Amesema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kupanua fursa za elimu ya juu kwa wanafunzi wenye sifa, kutambua juhudi zao na kupunguza vikwazo vya kifedha vinavyoweza kuwazuia kuendelea na masomo.

Aidha, ameitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha ufaulu na kukabiliana na changamoto ya wanafunzi wanaopata Daraja Sifuri na Daraja la Nne, huku akiwataka wadau wa maendeleo kuongeza mchango wao katika sekta ya elimu.
Vilevile, amewapongeza walimu kwa mchango wao katika kuimarisha ufaulu na kuwataka kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kujituma. 

Amewataka pia wazazi na walezi kusimamia nidhamu za watoto wao na kuwajengea utamaduni wa kusoma ili kuimarisha ubora wa elimu Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here