Rais Dkt. Mwinyi ataja siri ya maendeleo na ustawi Zanzibar

ZANZIBAR- Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezitaka taasisi za kidini kuendelea kuhamasisha amani, umoja na utulivu, akisisitiza kuwa ni misingi muhimu ya maendeleo na ustawi wa wananchi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mhasham Baba Askofu Lameck Paul Ndomba, Askofu wa 11 wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar, Ikulu Zanzibar.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Oktoba 21, 2026 alipokutana na Mhasham Baba Askofu Lameck Paul Ndomba, Askofu wa 11 wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar, Ikulu Zanzibar.
Amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali na taasisi za kidini katika kuimarisha upendo, mshikamano na kutekeleza shughuli za maendeleo kwa manufaa ya wananchi.

Kwa upande wake, Askofu Ndomba amesema, yupo tayari kushirikiana na Serikali katika kuhamasisha amani, maelewano na maridhiano, akieleza kuwa jamii yenye amani na umoja ina mazingira bora ya kushiriki katika shughuli za maendeleo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Mhasham Baba Askofu Lameck Paul Ndomba, Askofu wa 11 wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar, Ikulu Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here