Elimu ya Nishati Safi yawafikia wanawake vijijini nchini Tanzania

IRINGA- Wizara ya Nishati imeendelea kutoa elimu kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa makundi mbalimbali ya wananchi, safari hii elimu hiyo imewafikia wanawake wanaoshiriki Jukwaa la Kitaifa la Wanawake Wanaoishi Vijijini linalofanyika katika Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa.
Mmoja wa wanawake wanaoishi vijijini akichangia mada kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia katika jukwaa hilo linalofanyika wilayani Kilolo, Iringa.

Elimu hiyo imetolewa ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa nishati hiyo katika kulinda afya na kuhifadhi mazingira.
Akizungumza katika jukwaa hilo, Mjiolojia kutoka Wizara ya Nishati, Nsajigwa Mwambumbuli, amesema kuwa matumizi ya nishati safi ya kupikia yanapaswa kupewa kipaumbele katika kaya, hususan za maeneo ya vijijini, ili kupunguza changamoto zinazohusiana na matumizi ya nishati zisizo safi na kuchangia katika uhifadhi endelevu wa mazingira.

Katika hatua nyingine, Mwambumbuli amewahimiza wananchi wa Wilaya ya Kilolo kuchagua na kutumia nishati safi ya kupikia inayopatikana katika maeneo yao, ikiwemo mkaa mbadala na teknolojia nyingine zinazofaa kwa matumizi ya kupikia, ili kurahisisha mabadiliko ya matumizi ya nishati katika kaya.
Kwa upande wake, Bi. Saida Mgeni ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa amesisitiza wanawake kuhama katoka matumizi ya kuni na mkaa na kuhamia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia,ili kupata nafasi ya kujiunga na vikundi mbalimbali vya uwezeshaji vya wanawake wilayani humo.

Ameeeleza kuwa, ni muhimu kwa wanawake waishiyo vijijini kubadilika na kuenda na wakati katika matumizi ya nishati safi ya kupikia ambayo ni nafuu na inatunza mazingira.
Jukwaa hilo la Kitaifa la Wanawake Wanaoishi Vijijini limebeba kaulimbiu isemayo “Mwanamke wa Kijijini: Nguvu ya Uzalishaji, Chachu ya Ustawi na Maendeleo ya Taifa Kuelekea Dira 2050.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here