RUVUMA- Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma imetangaza nafasi za kazi za kujitolea kwa mkataba kwa Watananzania wenye sifa na uwezo.
Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Tangazo lenye Kumb. Na. TDC.L.40/31/67 la Oktoba 16, 2026 lililotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Namsifu S. Balula linaeleza nafasi hizo ni Daktari Daraja la II, nafasi 03, na Afisa Muuguzi Msaidizi II, nafasi 10.
1.0 DAKTARI II (NAFASI 03)
a) Sifa za Mwombaji
Kuajiriwa mwenye shahada ya Udaktari/ Daktari wa meno toka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na serikali na waliosajiliwa na Chama cha Madaktari Tanzania.
b) Kazi na majukumu:
i. Kufanya kazi zote za matibabu hospitalini zinazohusiana na magonjwa mbalimbali katika fani husika.
ii. Kupanga, kusimamia na kutathimini huduma katika wilaya au mikoa
iii. Kufundisha wanafunzi katika vyuo vya afya vilivyo eneo lake la kazi
iv. Kuchunguza, kufuatilia na kuzuia milipuko ya magonjwa
v. Kutayarisha elimu ya kujiendeleza ya watumishi wa afya.
vi. Kufundisha na kuelekeza watumishi walio chini yake
vii. Kusimamia wafanyakazi walio chini yake.
viii. Kubuni, kuendesha na kutathimini utafiti na kusambaza matokeo
ix. Kubuni na kutayarisha mikakati ya kuinua ubora wa huduma ya fani yake
x. Kutoa huduma za outreach katika kanda
xi. Kutoa huduma za medical legal
xii. Kushiriki katika kutengeneza na kusimamia utekelezaji wa Sera na Mipango ya Serikali juu ya afya
xiii. Kushauri wizara kuhusu uendeshaji wa shughuli za afya nchini.
xiv. Kushiriki katika kamati ya jopo la madaktari (medical board) kwa ajili ya kustaafisha wafanyakazi kwa matatizo ya kiafya.
xv. Kutayarisha mitaala ya elimu ya kujiendeleza ya watumishi wa afya.
xvi. Kuandaa mipango na makisio ya bajeti ya huduma za afya
xvii. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
Mshahara: Daktari wa Mkataba atalipwa posho ya Tsh. 900,000/= kwa mwezi.
3.0 AFISA MUUGUZI MSAIDIZI II (NAFASI 10)
a) Sifa za kuajiriwa moja kwa moja
Kuajiriwa wenye Stashahada (Diploma) ya Uuguzi, kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, waliosajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania.
b) Kazi na Majukumu:
i. Kutoa huduma za uuguzi
ii. Kukusanya takwimu muhimu za afya.
iii. Kuwaelekeza kazi wauguzi walio chini yake
iv. Kuelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya
v. Kutoa huduma za kinga na uzazi
vi. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake
Mshahara: Afisa Muugizo Msaidizi wa Mkataba atalipwa posho ya Tsh. 400,000/= kwa mwezi.
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha ulemavu walionao.
iii. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya barua pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
iv. Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho cha elimu na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika Postgraduate/ Degree/ Advanced Diploma/ Diploma / Certificate- Cheti cha Mtihani wa kidato cha nne na cha Sita, Computer Certificate- Vyeti vya kitaaluma (Proffessional Certificate from Respective Boards).
v. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
vi. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET).
vii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokua kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
viii. Waombaji wa kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
ix. Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kugushi watachukuliwa hatua za kisheria.
x. Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Ki Apo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.
xi. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 29 Oktoba saa 9:30 alasiri 2026.
Barua zote zitumwe kwa njia ya posta kwa:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
48 Barabara ya Nalasi, S.L.P 275, 57682
Tunduru.
Mawasiliano:
Simu +25502680004,
Nukushi +25502680208,
Barua pepe: info@tundurudc.go.tz,
Tovuti: http://www.tundurudc.go.tz
Tags
Ajira Tunduru
Habari
Halmashauri ya Tunduru
Kazi za Kujitolea
Matangazo
Nafasi za Kazi
Ruvuma
Tangazo
