BANGKOK- Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba ametunukiwa tuzo maalum ya Magavana wa Benki Kuu waliopata Daraja A kwa mwaka 2026 na taasisi ya kimataifa ya Global Finance.
Ni kwa kutambua mchango wake katika usimamizi wa sera ya fedha, sekta ya fedha na kukuza huduma jumuishi za fedha.
Tuzo hiyo imetolewa leo Oktoba 17, 2026 jijini Bangkok nchini Thailand, wakati wa mikutano ya mwaka ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Kundi la Benki ya Dunia (World Bank Group).
Ni heshima kubwa kwa Benki Kuu na Taifa kwa ujumla kupata tuzo hiyo, kwa kuwa inaakisi mchango wa BoT katika kusimamia sera ya fedha na kuendeleza sekta ya fedha iliyo imara na jumuishi.
Tags
Bangkok
Benki Kuu ya Tanzania
Gavana Emmanuel Tutuba
Habari
Kimataifa
Tuzo ya Kimataifa
Uchumi na Fedha
