Elimu ya Mpiga Kura: INEC yatoa vibali kwa Asasi 7 Chamwino

NA DIRAMAKINI

TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetoa kibali kwa taasisi na asasi za kiraia saba (07) kutoa elimu ya mpiga kura na vibali kwa asasi tatu (03) kuwa waangalizi wa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Chamwino na Uchaguzi wa Madiwani katika Kata 11 za Tanzania Bara.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 06, 2026 jijini  Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Uchaguzi INEC, Bw. Ramadhani Kailima.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha Tume kilichofanyika leo Oktoba 6, 2026 kwa mujibu wa kifungu cha 10(1)(h) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 292, kikisomwa pamoja na Kanuni ya 22(4) ya Kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi za Mwaka 2024.

Aidha, vibali vya uangalizi wa uchaguzi vimetolewa kwa mujibu wa kifungu cha 85(4) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Sura ya 343, kikisomwa pamoja na kanuni ya 13(4) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za Mwaka 2025.

Tume imetumia fursa hiyo kuzipongeza taasisi na asasi zote zilizofanikiwa kupata vibali hivyo na kutoa wito kwao kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu na kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya uchaguzi.

Orodha ya taasisi zilizopata vibali:

A: Kutoa Elimu ya Mpiga Kura (07)

1. New Hope Community Development Organization

2. Save The Mother And Children Of Central Tanzania

3. Morogoro Saving The Poor Organization

4. Njombe Paralegals Centre

5. Patronage For Persons With Disabilities

6. Tanzania Child Welfare

7. The Mwalimu Nyerere Memorial Academy

B: Kuwa Waangalizi wa Uchaguzi (03)

1. Njombe Paralegals Centre

2. Save The Mother And Children Of Central Tanzania

3. Tanzania Child Welfare

Uchaguzi Mdogo katika Jimbo la Chamwino, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino na katika kata 11 unatarajiwa kufanyika hivi karibuni kufuatia nafasi wazi zilizojitokeza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here