Jinsi ya kubaini noti halali: BoT yatoa elimu Katavi na Rukwa

KATAVI-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa elimu kwa umma kuhusu namna ya kutambua alama za usalama zilizopo kwenye noti za Tanzania, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu utambuzi wa noti halali na kuwawezesha kujikinga dhidi ya matumizi ya fedha bandia.
Elimu ya kutambua alama za usalama zilizopo kwenye noti za Tanzania ikiendelea.
Kampeni hiyo ilifanyika Mpanda, mkoani Katavi, kuanzia tarehe 14 hadi 25 Septemba 2026, ambapo elimu ilitolewa katika shule mbalimbali za msingi na sekondari.

Elimu hiyo pia ilitolewa kwa Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu suala hilo.
Aidha, katika kuhakikisha elimu hiyo inawafikia wananchi kutoka makundi mbalimbali kwenye jamii, BoT ilitoa elimu hiyo kwa watu wenye ulemavu wa kusikia kupitia Taasisi ya Maendeleo kwa Viziwi Tanzania (TAMAVITA), Sumbawanga, mkoani Rukwa. Elimu hiyo ilitolewa Septemba 29, 2026.
Mpango huo ni sehemu ya juhudi endelevu za Benki Kuu za kutoa elimu ya fedha kwa makundi mbalimbali ya jamii na kuhakikisha wananchi wanakuwa na uelewa sahihi kuhusu alama za usalama zilizopo kwenye noti za Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here