Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 22, 2026

Soma habari zote muhimu leo Oktoba 22, 2026 kutoka katika magazeti makubwa ya Tanzania kama Mwananchi, HabariLeo, Majira, Nipashe, Zanzibar Leo, Raia Mwema, Mwanahalisi, Uhuru, Pambazuko, Jamhuri na mengineyo kila siku bila malipo.
MWANANCHI, Alhamisi, Oktoba 22, 2026 - Gazeti linaeleza kuwa, wakongwe wa CCM wataka hatua dhidi ya rushwa ndani ya chama, Serikali yajipanga kukabiliana na athari za El Nino, Kiongozi wa Chadema John Pambalu apandishwa kizimbani kwa uhaini, huku LATRA ikionya juu ya nauli za usiku na kukatisha ruti zinazowatesa abiria.
MWANANCHI HURU, Alhamisi, Oktoba 22, 2026 - Gazeti linaongoza na habari kuwa EU yarejesha ufadhili wa bilioni 461 kwa Tanzania baada ya kuridhishwa na hatua za Serikali, fedha zitakazoelekezwa kwenye miundombinu na mabadiliko ya tabianchi, Rais Samia aongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu Dar es Salaam, Tanzania yapiga hatua kudhibiti rangi zenye sumu ya risasi kutoka asilimia 85 hadi 13, na Serikali ya Zanzibar kufadhili wanafunzi 143.
WAMACHINGA, ALHAMISI OKTOBA 22, 2026 - Gazeti linaongoza na kauli ya Mwigulu kuwa ukiwekeza Tanzania umefikia watu milioni 170 EAC, akiwa anaongoza mjadala kuhusu uwekezaji kwenye kilimo biashara, huku MNH ikipambana na saratani ya uso, kinywa, shingo kwa wagonjwa 15 kufanyiwa upasuaji, na Rais Samia aongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu.

WAMACHINGA SPOTI- Gazeti linaripoti Simba yaichapa De Agosto, Doumbia atakata, Yanga yatinga makundi CAF, huku Drogba akisema Tanzania chini ya Makonda itafanya vizuri katika michezo na Kocha wa Bandari hajaridhishwa na timu yake.
MAJIRA, Alhamisi, Oktoba 22, 2026 - Gazeti linaongoza na habari kuwa TRA yawatoa wasiwasi walipakodi hapa nchini ikisisitiza hakuna biashara zitakazofungwa kwa sababu ya kodi, Serikali na wadau wa kodi kushirikiana Dira ya Taifa, Waziri Mkuu Mwigulu aongoza mjadala kuhusu uwekezaji, na robo mwaka yakutanisha Wizara ya Maliasili na Utalii.

MAJIRA MICHEZO- Gazeti linaripoti Simba SC yaikung'uta kinyama 15 de Agosto ikiichapa 6-1 ambapo Ibrahim Doumbia aliibuka nyota kwa kufunga mabao mawili, huku watalii kushudia AFCON 2027 msituni baada ya TFS kukamilisha ukarabati.
HabariLEO, Alhamisi, Oktoba 22, 2026 - Gazeti linaongoza na Mwigulu avuta mitaji kilimo akieleza mvuto wa Tanzania soko la watu milioni 170 na kuishukuru IFAD, Serikali yasema hakuna mgonjwa wa Ebola Tanzania, Dereva bodaboda afa akishindana na mwenzake, na TMA yasema El Nino ipo, tena kubwa.

HabariLEO Michezo, Alhamisi, Oktoba 22, 2026 - Gazeti linaongoza na Doumbia aanza kazi Simba, Kazimzumbwi kutangaza utalii Afcon 2027, TAFF yataja kikosi Tembo Queens, na UEFA yambana Infantino.
Zanzibar Leo, Alhamisi, Oktoba 22, 2026 - Gazeti linaongoza na Dk. Mwinyi ashusha neema kwa wanafunzi akiwaongezea wigo mikopo kidato cha sita, Dk. Pembe asema Serikali imepunguza ada za leseni maudhui mitandaoni, ZHESLB yatoa mikopo kwa wanafunzi 4,718, na Watuhumiwa tisa mauaji ya mwanafunzi Raiyan wakamatwa.

Zanzibar Leo Michezo, Alhamisi, Oktoba 22, 2026 - Gazeti linaongoza na Yanga yatinga makundi CAFCL, Doumbia afunga Simba ikiichakaza 15De Agosto 6-1, Azam FC yaivutia pumzi ZED, na Ligi kuu mpira wa Wavu kuanza Oktoba 25.
Nipashe, Alhamisi, Oktoba 22, 2026 - Gazeti linaongoza na Kigogo mwingine CHADEMA kortini shtaka la uhaini ambapo John Pambalu aliyekamatwa Arusha amepandishwa kizimbani Dar es Salaam, Watoto wa Rwakatare wafikishana pabaya mahakamani juu ya mirathi, Waliopata Daraja la kwanza pointi 3-5 kusomeshwa bure, na tisa mbaroni tuhuma za mauaji ya mwanafunzi Pemba.

Nipashe Michezo, Alhamisi, Oktoba 22, 2026 - Gazeti linaripoti Barker apagawa na mabao ya Doumbia ambaye ametupia mbili Simba ikitakata michuano ya CAF, Yanga na Simba 'moto' kwenye mechi za nyumbani, na Ten Hag akisema Ronaldo 'aliimaliza' United.
Taifa Tanzania, Alhamisi, Oktoba 22, 2026 - Gazeti linaongoza na Serikali yatoa tahadhari ya Ebola, Wizara ya Nishati yawasilisha utekelezaji wa bajeti sekta ndogo ya umeme na nishati jadidifu, Wafugaji 43 vinara wa migogoro kusakwa popote walipo, na Ukiwekeza Tanzania umewafikia watu milioni 170 - Dk. Mwigulu.

Taifa Tanzania Michezo, Alhamisi, Oktoba 22, 2026 - Gazeti linaongoza na Mashabiki Simba SC wamlilia Doumbia aliyeingia akitokea benchi na kupiga 2 Mnyama aibuka na ushindi wa mabao 6-1, Ibrahimu Class kutetea mkanda Kimataifa Nov. 13, Kiruswa Jimbo Cup yaibua vipaji wanne kupelekwa Hispania, na Novatus aifungia bao Goztepe.
Tanzania Leo, Alhamisi, Oktoba 22, 2026 - Gazeti linaongoza na maono ya Dkt. Samia kukuza uchumi Afrika, Dkt. Samia aongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Dar es Salaam, Zanzibar yaongeza bilioni 10 bajeti ya mikopo elimu ya juu, na Mwigulu asema ukiwekeza Tanzania umewafikia watu milioni 170.

Spoti Tanzania Leo, Alhamisi, Oktoba 22, 2026 - Gazeti linaripoti Doumbia atoa gundu, atupia mbili Simba akitambulisha staili mpya ya ushangiliaji, Mo Dewji aweka Sh 400Mil kwa mastaa Simba, Mwenda atupwa nje Yanga SC, na Pigo PSG, Kvaratskhelia nje msimu mzima.
MWANA SPOTI, Alhamisi, Oktoba 22, 2026 - Gazeti linaongoza na NGUVU MOJA, DAIMA MBELE huku Simba ikiichapa Agosto 6-1 na Doumbia atupia vaibu kila kona, Yanga yaichapa CFFA 4-1 kwenye Azam Complex na Mwalimu kung'ara, huku Harmonize na Rayvanny wakivunja 'ukuta WCB' na jezi ya Messi kitambaa vyaibwa.
MwanaHabari, Alhamisi, Oktoba 22, 2026 - Gazeti linaongoza na habari kuwa, Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji kwenye kilimo, Dkt. Mwigulu awataka wenye mitaji kuwekeza ili kufikia soko la watu milioni 170 Afrika Mashariki na Kati, Rais Samia aongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu Dar es Salaam, Biashara bunifu za Tanzania zinachukua fursa kubwa Marekani na wazazi/walezi wahimizwa kuwalea watoto katika mazingira salama.

MwanaHabari Michezo, Alhamisi, Oktoba 22, 2026 - Gazeti linaripoti Simba yaichapa De Agosto 6-1 huku Doumbia akiwa 'wa moto', Yanga 'yaibonda' CFFA ikitinga makundi CAF, Drogba ampongeza Makonda kusimamia michezo yote nchini, na Feisal kuzigonganisha timu dirisha dogo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here