Simba SC yaichakaza 15 de Agosto mabao 6-1 klabu Bingwa Afrika

NA DIRAMAKINI

SIMBA Sports Club (Simba SC) ya jijini Dar Es Salaam, Tanzania imeanza vema kampeni ya kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa barani Afrika baada ya kuichapa 15 de Agosto kutoka Equatorial Guinea mabao 6-1 katika mchezo uliopigwa Oktoba 21, 2026 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Nathaniel Chilambo alianza kuifungia Simba dakika ya 42, kabla ya Elie Mpanzu kuongeza bao la pili dakika ya 55.

Aidha, Ibrahim Doumbia alifunga bao la tatu dakika ya 64 na kuongeza la nne dakika ya 81, huku Keletso Makgalwa akitikisa nyavu dakika ya 71 na Anicet Oura akafunga bao la sita dakika ya 82.

Matokeo hayo yameiweka Simba katika nafasi nzuri ya kusonga mbele na kutinga hatua ya makundi, ingawa bado inahitaji kuthibitisha nafasi hiyo katika mchezo wa marudiano utakaopigwa wiki hizi.

Doumbia ameweka rekodi muhimu katika safari yake ya Simba kwa kufunga mabao yake ya kwanza tangu asajiliwe na klabu hiyo.

Wakati huo huo, mchezo wa marudiano utakapigwa Jumapili Oktoba 24 katika Uwanja wa Uhuru saa 10 jioni jijini Dar Es Salaam.

Jedwali la wafungaji mabao ya Simba SC dhidi ya 15 de Agosto

Mchezaji (Simba SC)Dakika ya BaoHatua ya Mchezo
Nathaniel Chilambo42'Bao la Kwanza
Elie Mpanzu55'Bao la Pili
Ibrahim Doumbia64', 81'Bao la Tatu & la Nne
Keletso Makgalwa71'Bao la Tano
Anicet Oura82'Bao la Sita

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here