NA DIRAMAKINI
MSIMAMO wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu wa 2026/27 umeendelea kuonesha ushindani mkubwa huku Simba SC ikiongoza kwa pointi 24 baada ya mechi nane.
Kwa mujibu wa msimamo uliotolewa Oktoba 24, 2026 na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB), Simba SC imepata ushindi katika mechi zote 8, ikiwa na mabao 19, kufungwa 4, tofauti ya mabao +15 na pointi 24.
Nafasi ya pili ni ya Young Africans SC yenye pointi 19 baada ya mechi 8, ushindi 6, sare 1 na kipigo 1, mabao 17-4, tofauti +13.
Azam FC iko nafasi ya tatu kwa pointi 17 baada ya mechi 8, ushindi 5, sare 2 na kipigo 1, mabao 13-7, tofauti +6.
JKT Tanzania iko nafasi ya nne kwa pointi 16 baada ya mechi 9, ushindi 5, sare 1 na kipigo 3, mabao 12-12, tofauti 0.
Dodoma Jiji inafunga nafasi tano na pointi 14 baada ya mechi 8, ushindi 4, sare 2 na kipigo 2. Katika kundi la kati, Polisi Tanzania na Namungo FC zote zina pointi 12, zikiwa nafasi ya sita na saba kwa mtiriko huo.
Polisi Tanzania imecheza mechi 9, sare 3, ushindi 3, kipigo 3, mabao 12-11, tofauti +1. Namungo FC nayo imecheza mechi 9, ushindi 4, kipigo 5, mabao 9-12, tofauti -3.
Mashujaa FC iko nafasi ya nane na pointi 12 baada ya mechi 8, ushindi 4 na kipigo 4, mabao 9-13, tofauti -4. Singida Black Stars iko nafasi ya tisa kwa pointi 11 baada ya mechi 8, ushindi 3, sare 2, kipigo 3, mabao 14-11, tofauti +3.
Msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa Oktoba 24, 2026.

Msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa Oktoba 24, 2026.
Mbeya City iko nafasi ya kumi kwa pointi 10 baada ya mechi 8, ushindi 3, sare 1, kipigo 4, mabao 8-9, tofauti -1.
Coastal Union iko nafasi ya kumi na moja kwa pointi 10 baada ya mechi 9, ushindi 3, sare 1, kipigo 5, mabao 8-13, tofauti -5.
TRA United SC iko nafasi ya kumi na mbili kwa pointi 7 baada ya mechi 8, ushindi 1, sare 4, kipigo 3, mabao 6-7, tofauti -1.
Geita Gold iko nafasi ya kumi na tatu kwa pointi 7 baada ya mechi 8, ushindi 2, sare 1, kipigo 5, mabao 9-15, tofauti -6.
Pamba Jiji FC iko nafasi ya kumi na nne kwa pointi 6 baada ya mechi 9, ushindi 1, sare 3, kipigo 5, mabao 10-15, tofauti -5.
Kagera Sugar iko nafasi ya kumi na tano kwa pointi 6 baada ya mechi 9, ushindi 1, sare 3, kipigo 5, mabao 9-17, tofauti -8.
Fountain Gate inafunga msimamo nafasi ya kumi na sita na pointi 5 baada ya mechi 8, ushindi 1, sare 2, kipigo 5, mabao 4-12, tofauti -8.
Nafasi za mwisho mbili, 15 na 16, ni za kushuka moja kwa moja daraja, wakati nafasi ya 13 na 14 ni za playoff na nafasi nyinginezo kwa mujibu wa msimamo huo.
