Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu akutana na Rais wa AGRA nchini Marekani

DES MOINES- Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amekutana na Rais wa AGRA, Bi. Alice Ruhweza, na kueleza hatua zinazochukuliwa na Tanzania kuimarisha kilimo na kuwawezesha vijana kushiriki katika sekta hiyo.
Mazungumzo hayo yamefanyika Oktoba 21, 2026, kando ya Mkutano wa Kimataifa wa Norman E. Borlaug (Borlaug Dialogue) jijini Des Moines, Jimbo la Iowa, Marekani. Waziri Mkuu anashiriki mkutano huo akimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Dkt. Mwigulu amesema, Serikali inaongeza uwekezaji katika umwagiliaji, uzalishaji wa mbegu bora, utafiti, huduma za ugani, maghala na miundombinu ya kuchakata mazao.
Aidha, amesema Tanzania inaendelea kushughulikia vikwazo vinavyowakabili vijana katika kilimo kwa kuwawezesha kupata ardhi, kuwapatia mafunzo na kuwaunganisha na benki ili kupata mitaji ya kununua mbegu, zana na pembejeo nyingine.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here